Jumamosi 27 Septemba 2025 - 07:06
Mapambano na Israel ni mapambano ya Kitamaduni yanayo endelea, na Muqawama haujashindwa na kamwe hautashindwa

Hawza/ Sheikh Ali al-Khateeb amesisitiza kwamba jamii ya Lebanon, pamoja na kuwa na tofauti za kimadhehebu na kidini, bado ni jamii moja yenye mshikamano, na msimamo wake unapaswa kuwa wa umoja katika kukabiliana na adui mwovu wa Kizayuni wa Kiyahudi ambaye analenga mamlaka, umoja na uhai wetu.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha shirika la habari Hawza, Sheikh Ali al-Khateeb, Makamu wa Rais wa Baraza Kuu la Kiislamu la Kishia Lebanon, katika hafla iliyoandaliwa na Halmashauri ya Jiji la Labbaya katika Husayniyya ya mji huo kwa kuhudhuriwa na Hisham Hassan, kiongozi wa Hizbullah huko Bekaa ya Magharibi, wawakilishi wa Harakati ya Amal, viongozi wa kisiasa, kielimu, kimiji pamoja na wanafunzi waliotunukiwa na wakaazi wa mji huo waliopita mitihani yao rasmi kwa mafanikio, alisisitiza kuwa jamii ya Lebanon, pamoja na wingi wa madhehebu na dini, bado ni jamii moja, na msimamo wake ni lazima uwe mshikamano katika kukabiliana na adui mwovu wa Kizayuni ambaye analenga mamlaka, mshikamano na uhai wetu.

Sheikh al-Khateeb aliongeza kuwa: Hata hivyo, watoto wa Muqawama walimkabili, waliilinda Lebanon, wakazipinga njama zake na wakamzuia asipate ushindi wowote.

Akaeleza kuwa: Adui wa Kizayuni alidhani anaweza kuishinda Lebanon, lakini kuanzia pale tu alipojikuta amekabiliana na wapiganaji wa Muqawama mipakani katika Kafr Kila, Mays al-Jabal, Kafr Shuba na maeneo mengine, alitambua kwamba hawezi kusonga mbele hata kwa mita moja ndani ya ardhi ya Lebanon, na maamuzi yake yalishindwa mbele ya uimara wa Muqawama.

Makamu wa Rais wa Baraza Kuu la Kiislamu la Kishia Lebanon alisisitiza: Baadhi ya watu wa ndani walijaribu kwa njia ya kuubana Muqawama na kuunyang’anya silaha zake, kufanikisha kile ambacho adui alishindwa kukifanikisha, lakini ukweli umeonesha kwamba Muqawama haujashindwa kijeshi wala kisaikolojia, mazingira yake bado ni thabiti, na Lebanon muda wa kuwa Muqawama upo, haitaweza kushindwa.

Sheikh al-Khateeb aliwakosoa wale waliotegemea diplomasia au uungaji mkono wa Marekani na kuuliza: Huo uungaji mkono upo wapi leo, hali ya kuwa uvamizi wa Kizayuni umefika kwenye moyo wa Ghuba na Doha, yenye kukibeba kituo kikubwa cha Marekani? Uongo wa madai kwamba hatari kwa Waarabu inatoka Iran au Muqawama sasa umefichuka, huku ukweli ukiwa kwamba hatari halisi ni Israel na wale walio nyuma yake.

Akaongeza: Kile ambacho adui alikitafuta kilikuwa ni kuuingiza ulimwengu wa Kiarabu kwenye mizozo ya ndani na kuugawa kuwa mataifa ya kimadhehebu, lakini tajriba imeonesha kwamba ulinzi wa kweli unaweza tu kutoka kwa watoto wa Umma wenyewe na kwa mshikamano na ushirikiano wao katika kumkabili adui.

Makamu wa Rais wa Baraza Kuu la Kiislamu la Kishia Lebanon aliwataka Waarabu na Waislamu watambue kwamba mapambano na Israel siyo mapambano ya ardhi au maslahi, bali ni mapambano ya kimaendeleo na ya jumla juu ya fikra, utamaduni, thamani, historia na familia, na mauaji, njaa na uharibifu ambayo adui anayatekeleza huko Ghaza si chochote ila ni kioo kinachoakisi uhalisia wa "utamaduni wa Magharibi."

Sheikh Ali al-Khateeb alisisitiza kuwa: Muqawama umeshinda; kwa sababu uliuelewa ukweli wa mzozo. Huu sio tu mzozo wa kijeshi unaotegemea uwiano wa nguvu za kimaada, bali ni mapambano ya irada na utamaduni. Na kwa sababu hii ndio maana uliweza kuyashinda malengo ya adui na kuzuia ardhi isivamiwe, leo, pamoja na ugumu wa hatua hii, mapambano haya hayajamalizika, bali bado ni mapambano yanayoendelea na yanayohitaji subira na irada.

Akamalizia kwa kusisitiza kwamba matumaini yapo kwa vizazi vipya ambavyo vimelelewa kwa utamaduni wa Muqawama na ushindi, na ambavyo vitabeba bendera ya kuitetea heshima ya Lebanon, Palestina na Umma katika misimamo yao.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha